Jumanne 16 Desemba 2025 - 22:02
Ayatullah Hosseini Bushehri: Hawza Inaenda Sambamba na Mabadiliko

Hawza/ Rais wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza alisema: Matokeo ya shughuli za vituo vyetu vya kielimu yanapaswa siku zote kuwepo juu ya meza za viongozi. Haitoshi kujitosheleza kwa kuwasilisha vitabu na makala katika maonesho na matamasha.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Farhad Abbasi, Naibu wa Utafiti wa Hawza, pamoja na kundi la wakurugenzi na viongozi wa naibu huu, walifika katika ofisi ya Jumuiya ya Walimu wa Hawza na kukutana pamoja na Ayatullah Sayyid Hashim Hosseini Bushehri, ambapo walifanya naye mazungumzo.

Ayatullah Hosseini Bushehri, katika mkutano huu uliofanyika kwa mnasaba wa Wiki ya Utafiti, akitoa pongezi kutokana na juhudi za Ayatullah A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza Iran, Baraza Kuu la Hawza na viongozi wengine wa kihawza katika suala la utafiti, alisisitiza kwa kusema: Mtazamo huu tunauhodhi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Mungu amhifadhi), ambaye kwa uelewa kamili hutoa maelekezo na pia tahadhari.

Hawza inaenda sambamba na mabadiliko

Akiashiria shughuli za utafiti za Hawza kupitia Kituo cha Utafiti wa Kompyuta cha Sayansi za Kiislamu (Noor), jumuiya za kielimu, Tamasha la Allama Hilli (rehma ya Mungu iwe juu yake) na Tuzo ya Kitabu Bora cha Mwaka, alisema: Haya yote yanaonesha kuwa Hawza haija simama, bali inaenda sambamba na mabadiliko.

Imam wa Swala ya Ijumaa, akitaja umuhimu wa watafiti na wanafikra wa kihawza kuzingatia ujumbe wa “Hawza inayoongoza na iliyo mstari wa mbele”, alibainisha: Tuna adui ambaye anajaribu kutushinda katika vita vya wazi na vya fikra (vita laini), na kutupokonya fikra na mawazo; kwa hiyo hatupaswi kupuuza kujibu mahitaji ya kizazi cha vijana na jamii.

Akiisisitiza umuhimu wa kuhuisha lugha na istilahi za utafiti katika Hawza za Elim, alisema: Kadiri tunavyoweza, ni lazima tuhuishe lugha za tafiti zetu, na tuyawasilishe maudhui ya vitabu vya wanazuoni wakubwa kwa mifumo mipya.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis-e Khobregan-e Rahbari) akisisitiza umuhimu wa kutekelezwa kwa vitendo kwa matokeo ya shughuli za tafiti katika uongozi wa nchi, alisema: Mfumo wa Kiislamu leo unahitaji utatuzi wa matatizo.

Akiashiria matatizo ya kiuchumi na majeraha ya kijamii, aliongeza: Ni lazima tufanye tafiti za kina za kuchambua matatizo haya, kisha tuyawasilishe matokeo yake kwa taasisi zinazofanya maamuzi na zinazounda sera.

Matokeo ya shughuli za kielimu yanapaswa kuwa juu ya meza za viongozi

Ayatullah Hosseini Bushehri, akiwahutubia viongozi wa tafiti za Hawza, aliongeza: Matokeo ya shughuli za vituo vyetu vya kielimu yanapaswa siku zote kuwa juu ya meza za viongozi. Haitoshi kujitosheleza kwa kuwasilisha vitabu na makala kwenye matamasha. Bidhaa hizi za kielimu zinapaswa kuchukua nafasi yake katika uendeshaji na uongozi wa jamii, ili nafasi ya kielelezo ya Hawza idhihirike wazi.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha