Shirika la Habari la Hawza - Imam Zaynu al-Abidin (a.s) katika Sahifa Sajadiya anamsemesha Mwenyezi Mungu hivi:
«إِذَا هَمَمْنَا بِهَمَّیْنِ یُرْضِیکَ أَحَدُهُمَا عَنَّا وَیُسْخِطُکَ الْآخَرُ عَلَیْنَا، فَمِلْ بِنَا إِلَی مَا یُرْضِیکَ عَنَّا وَ أَوْهِنْ قُوَّتَنَا عَمَّا یُسْخِطُکَ عَلَیْنَا.»
Na kila mara tunapokutana na jambo moja ambalo linakuridhisha na lingine halikuridhishi, basi tupondoshe sisi katika lile ambalo litakalokuridhisha na utufanye dhaifu katika jambo lile ambalo linakukasirisha. (1)
Sherehe:
Binadamu, kila wakati anapata anakutana na changamoto zilizopo ndani na nje yake, kutokana na pande mbili za wema na ubaya.
Ingawa binadamu ameumbwa kuwa na uhuru wa kuchagua, amepewa vyombo vya utambuzi, ufanisi na ukuaji, na njia ya kuelekea kwake imeelekezwa na Mitume na Vitabu vya Mwenyezi Mungu, bado binadamu huyo anaweza kushawishiwa na matamanio ya nafsi yake au shetani, akashindwa kutumia vyema uhuru huu, vyombo vya utambuzi na uongofu kama inavyotakiwa, na kuingia kwenye njia ya upotevu. Badala ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu, yeye akajiletea hasira Yake.
Hivyo binadamu anahitaji neema nyingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nayo ni "Taufiqi" – neema ya kumsaidia kubaki katika njia ya kimungu ambayo ni njia ya furaha ya milele.
Katika riwaya kutoka kwa Imam Baqir (a.s) kuhusu tafsiri ya «لا حول ولا قوّة إلّا بالله» inasemwa:
«مَعْنَاهُ لاَ حَوْلَ لَنَا عَنْ مَعْصِیَةِ اَللَّهِ إِلاَّ بِعَوْنِ اَللَّهِ وَلاَ قُوَّةَ لَنَا عَلَی طَاعَةِ اَللَّهِ إِلاَّ بِتَوْفِیقِ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ.»
Maana yake ni kwamba hatuna uwezo wa kujiepusha na dhambi za Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na hatuna uwezo wa kumtii Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa taufiqi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. (2)
Kutokana na maana hii, Nabii Shuaib (a.s) katika Qur'an Tukufu anawasemesha Makafiri kwa kusema:
«وَمَا تَوْفِیقِی إِلَّا بِاللَّهِ.»
Na haikuwa Taufiq yangu isipokuwa ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake. (3)
Na bila shaka, kuomba taufiqi kutoka kwa Mwenyezi Mungu bila juhudi ni bure; kama ilivyoelezwa na Imam Rida (a.s):
«وَمَنْ سَأَلَ اَللَّهَ اَلتَّوْفِیقَ وَلَمْ یَجْتَهِدْ فَقَدِ اِسْتَهَزَأَ بِنَفْسِهِ.»
Kila mtu atakayemuomba Mwenyezi Mungu taufiqi na hakujibidiisha, basi atambue kwamba anajidhihaki mwenyewe. (4)
Rejea:
1. Sahifa Sajadiya, Dua ya Ishirini.
2. At-Tawhid, Juz. 1, Uk. 242.
3. Surah Hud, Ayah 88.
4. Bihar al-Anwar, Juz. 75, Uk. 356.
Imeandaliwa na Kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza.
Maoni yako