Jumatano 17 Desemba 2025 - 15:03
Licha ya Mashinikizo Yote, Muqawama Utaendelea Kumiliki Silaha

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Faisal Shukr alisisitiza kuwa; bendera ya muqawama itaendelea kuinuliwa, na silaha zake, licha ya mashinikizo yote, silaha zitaendelea kubakia mikononi mwa wapiganaji wa muqawama.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Faisal Shukr, msimamizi wa eneo la Beqaa ndani ya Hizbullah, katika mkutano wa maridhiano ulioandaliwa na Hizbullah katika sekta ya tatu (ya magharibi), kwa kuwakusanya baadhi ya wanafamilia wa Mashik, uliofanyika katika Majma‘ al-Imam al-Baqir (a.s) huko Al-Za‘arir – Bayt Mashik, alisisitiza kuwa bendera ya muqawama itaendelea kuinuliwa na silaha zake, licha ya mashinikizo yote, zitaendelea kubakia mikononi mwa wapiganaji wa muqawama.

Mkutano huu ulifanyika chini ya usimamizi wa Sayyid Shukr na Hasan Hamiya, msimamizi wa sekta ya tatu ya Hizbullah, na kwa ushiriki wa wanazuoni wa dini, familia za mashahidi, wanaharakati wa chama, wa kijamii na wa kikabila, pamoja na wawakilishi wa manispaa.

Hujjatul-Islam Shukr alisisitiza kuendelea na chaguo la muqawama hadi kufikiwa ushindi kamili na kumalizika kwa utawala wa Marekani katika eneo, na kufuatia hilo, kumalizika kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Alibainisha kuwa chaguo la muqawama ni chaguo la heshima na mamlaka ya kujitawala, na hakuna kurudi nyuma kutoka katika chaguo hilo.

Katika mkutano huu, Sayyid Shukr alisisitiza umuhimu wa suluhu (maridhiano) katika Uislamu na nafasi yake katika kuimarisha amani ya ndani na kudumisha uthabiti wa kijamii. Alieleza kuwa: utamaduni wa maridhiano na kuvumiliana ni nguzo muhimu katika kujenga jamii iliyoshikamana na yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha