Ijumaa 5 Desemba 2025 - 14:00
Watu Mashuhuri Wataka "Tumaini la Palestina" Aachiliwe Huru Kutoka Gerezani

Hawza/ zaidi ya watu mashuhuri mia mbili wametangaza kwamba wanataka kwa dhati kuachiliwa huru Marwan Barghouti, mmoja wa viongozi wa mapambano ya Palestina ambaye wataalamu wamempa jina la “Tumaini la Palestina”.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Marwan Barghouti, mwenye umri wa miaka 66, alifungwa gerezani baada ya kile ambacho wataalamu wa sheria wamekitaja kuwa ni kesi isiyo kamili na isiyo ya haki, na mpaka sasa ametumia miaka 23 gerezani.

Yeye ambaye wakati wa kukamatwa alikuwa mwakilishi wa bunge aliyechaguliwa, bado ndiye kiongozi anayependwa zaidi na Wapalestina, na kama chaguo la wananchi kwa urais huwa daima anaongoza katika kura za maoni zinazofanywa miongoni mwa Wapalestina.

Hilohilo limezua hofu hivi karibuni kwamba Serikali bandia ya Israel inajaribu kupitisha sheria mpya zitakazoiruhusu serikali hiyo dhalimu kutekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa wa Kipalestina sheria ambayo inaweza pia kumhusu Barghouti.

Kwa sababu hiyo, makundi mengi mashuhuri kupitia barua ya wazi yametaka aachiliwe huru. Miongoni mwa majina muhimu yaliyoorodheshwa ni pamoja na waandishi: Margaret Atwood, Philip Pullman, Zadie Smith na Annie Ernaux; pia wasanii na waigizaji kama Sir Ian McKellen, Benedict Cumberbatch, Tilda Swinton, Josh O’Connor na Mark Ruffalo; na Gary Lineker, mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu, pamoja na watu maarufu kama Sir Richard Eyre (mkurugenzi), Ai Weiwei (msanii mashuhuri), na mfanyabiashara bilionea Sir Richard Branson—wote wakiwa miongoni mwa waliodai kwa dhati kuachiwa huru Marwan Barghouti.

Chanzo: The Guardian

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha