Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha Shirika la Habari la Hawza, mkutano huu unaotambuliwa kuwa miongoni mwa mikutano mikubwa zaidi ya Waislamu Amerika Kaskazini, hufanyika katika kipindi cha mwisho wa juma, na lengo lake ni kufufua tafakuri ya kiroho katika jamii. Waandaaji wa tukio hili wanajitahidi kuweka miongozo ya vitendo kwa ajili ya maisha yenye sa‘ada katika zama za sasa.
Kwa takribani miongo miwili, mkutano wa kufufua Uislamu halisi umeendelea kutekeleza jukumu kuu katika kulea na kuimarisha jamii za Waislamu kote Amerika Kaskazini.
Kongamano hili limekuwa likionesha mfululizo wa mazingira ambayo ndani yake imani sahihi, akili na tajriba ya kuishi kwa usahihi hukutana, na jambo hili huwapa washiriki fursa ya kukuza kwa kina zaidi uelewa wao wa Uislamu, huku wakati huo huo wakilinganisha na kuoanisha dini na uhalisia wa dunia ya kisasa.
Mada ya jumla ya mihadhara inalenga maisha na hadithi za Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye na Aali zake), na pia wema na ukarimu wake huainishwa kama misingi endelevu ya maendeleo ya mtu binafsi na ya pamoja kwa wanadamu.
Baadhi ya vikao hivi pia huelezea historia ya Uislamu, kuanzia nyakati muhimu za mwanzo wa Uislamu hadi leo; lakini si kama matukio ya kihistoria tu, bali kama mfumo wa kivitendo wa kufafanua athari ya uongozi katika uendeshaji wa jamii wakati wa kufanya maamuzi ya kimaadili katika zama za kisasa.
Chanzo: ABOUT ISLAM
Maoni yako